NAMNA
NZURI YA KUOSHA NYWELE ZAKO
KUNA kitu muhimu kuhusu uoshaji wa nywele, nywele zako ambazo unataka zikae unavyotaka kulingana na kichwa chako ili uwe na uvuto wa haiba yake katika mambo yote yanayokuzunguka.
katika mazingira ya kawaida uoshaji nywele ni kitu cha kawaida na hivyo mara nyingi hatufikirii sana suala la kuosha nywele, si la kawaida tu mwenzangu? Lakini uoshaji nywele wa uhakika wenye makini kwa kutumia shampuu kunaweza kuleta mabadiliko makubwa katika muonekano na umetaji wa nywele zako na hata makuzi yake.
Ndio kusema uoshaji wa kutumia shampuu unaweza kabisa kukupa kile ambacho huwezi kukipata katika hali ya kawaida , muondoko wa ukaaji wa nywele baada ya kuosha.
Lakini kama hutajali tulijadili hili suala la uoshaji nywele ambalo ni la kawaida tu.Naama, la kawaida lakini lenye maana kubwa kwa watu wanaojijali.
Mimi nadhani haitaumkiza kama nikisema kwa ufupi fupi kuhusu hizi shampuu za kuonshea nywele, hizi shampuu ambazo unazipata dukani, kwenye dula la urembo.
Kwanza ni lazima utambue kwamba si kila shampuu inafaa katika kusuklia nyweleza ko (uoshaji) kwani nyingine huleta mushkeri hasa kama unaumwa eczema, hali ya kuchoma choma, uwasho wa nywele, mba au aina ya grisi katika ngozi ya nywele zako wakati wa kuzitengeneza.
Nataka kukuambia kwamba bidhaa zinazotokana na uasili husaidia sana kutengeneza utamu wa nywele kama kweli unaujua na mara zote hufanyakazi bora kwa aina zote za vichwa hata kama zina matatizo niliyotaja hapo juu.
Na pia huleta aina ya burudiko.
Mara zote tunapoosha nywele zetu huwa tunaharibu lakini kama utakuwa mwangalifu kwa kutumia shampuu zenye viambata vya asili (organiki-natural botanical)utakuwa na nafasi kubwa ya kuwa na nywele tamu na wewe kuondokana na adha za uchafu wa nywele unaotia 'wazimu'.
Kama utakuwa huna shampuu ile ya dukani ambayo ina aviambata vya asili nashauri utumie yai. yai ni kifaa kizuri kabisa cha kusafishia.tenganisha kiini cha yai kutoka katika uite mweupe. konga tofauti kisha changanya na taratibu zitumie kuzichanganya katika nywele ne kusukasuka. Acha kwa dakika tatu na kisha safisha kwa maji ya uvuguvugu si ya moto kwani ukitia maji ya moto yao litajikusanya maeneo fulani fulani kichwani halafu itakuwa shida.
Njia tano za kuosha nywele zako:
1.Inama katika beseni. Hii inasaidia kutoa nafasi ya ukaaji mzuri wa kuanza kusafisha nywele bila kuumiza shingo yako na pia kusaidia kuweka damu katika mzunguko unaotakiwa.
2.Tumia kikombe kimoja cha shampuu. Ikiwa nyingi italeta matatizo kidogo na kidogo pia haitatoa kitu kinachostahili. pakaza kwa kusukasuka kila mahali kichwani mwako kwa kuanzia mbele kwenda nyuma na kisha pembeni. Kwa nywele za grisi(mafuta) changanya shampuu na maji kidogo.
3. Tumia ncha ya vidole vyako kufika mwisho wa nywele na kuzimasaji vyema kuhakikisha kwamba shampuu inaingia katika ngozi ya kichwa. Safisha kwa raha kwani inatakiwa ujisikie raha kubwa wakati wa shughuli hii ya kusafisha nywele.
4.Hakikisha kwamba umesafisha sawasawa kichwa chako kisha unaondoa shampuu kwa maji..Kitu cha maana ni kuwa usafishaji lazima ufanyike kwa uangalifu mkubwa kwani baada ya kutia shampuu na kuipeleka kila mahali kuiondoa baada ya hapo ni kitu muhimu.Iondoe kwa maji na kisha kujihakikisha kwamba imeondoka, unastahili kukitia kichwa chako maji ya baridi kwa ajili ya kutoa busti zaidi.
5.Kausha nywele zako kwa taulo safi (kwepa kusugua nywele hizo kwa taulo).Kifunike kichwa na taulo hilo ili linyonye maji taratibu na baada ya hapo unaweza kutia kitu kinachotakiwa ili kuweka nywele za safi
MAISHA , MAPENZI, UREMBO
Maisha yetu ya kila siku yana vitu vingi sana, vizuri
kiasi kwamba unaweza furahi hadi ukajiuliza KWANINI NILICHELEWA kuanza????Na
kuna vingine ni vibaya, kiasi kwamba unaweza kulia hadi ukajutia kwanini
ulisema YES I DO.. njooni tuzunguze, tuongee, tushauriane,,tuone jinsi gani
tunaweza kuboresha maisha haya wote tukayafurahia
HAYA, KWA WALE WALIOHITAJI VITU NINAVYOTUMIA KATIKA KUJAZA,KUKUZA NA KUPENDEZESHA NYWELE ZANGU
Kwa
leo ninawaambia ni nini na tumia, ila nitaandaa picha za hivyo vitu pia ili
niwatumie wiki ijayo,
Dawa
ninayotumia ni Olive Oil, zipo za
aina tatu, na zote ni bidhaa za olive, na ambayo huwa naitumia sana ni ile
yenye picha ya mtoto kwenye box, ambayo ndani yake ina kikopo kidogo cha
steaming
Natumia
Avocado shampoo, ni nzuri sana, lakini
hata kama utaikosa kwenye haya masalon yetu waweza tumia shampoo yeyote ile,
mradi nywele zioshwe na zitakate, na pia tutumie conditioner, baada ya kuosha na shampoo,
conditioner inasaidia sana kulainisha nywele na kuzuia zisikatike wakati wa
kuchana, ni muhimu sana kuwa nayo, kama kwenye masalon yetu hakuna, basi nunua
kifumu au kopo lako then unakuwa ukienda salon unamimina kidogo unakwenda nayo,
Huwa
natumia mayonise steaming,
hii pia ziko za aina mbili, kuna le kubwa kabisa ambayo ni white cream, na kuna
kubwa kias ambayo ni dark cream, I mean cream iliyokolesa sanaaaaa,
Sasa
hii iliyo koleza sana ndio huwa natumia, na ninaitumia kila wiki, yani kila
juma pili lazima nifanye steaming
Baada
ya kuosha nywele zangu toka kwenye steamer kabla ya kupaka pinki lotion na
kuanza kuseti huwa napaka kwenye ngozi ile steaming iliyopo ndani ya
dawa, naipaka kwenye ngozi tu! Kisha inachanganywa, halafu ndio unapaka
pinki lotion kiasi tu(hii haioshwi, unasetia
Baada ya nywele
kukakuka huwa natumia Blue magic chafu, wenyewe
wauzaji wanaita blue magic ya chenga, inapakwa kwenye ngozi, na juu, kama
ukikosa tumia hata Venus, but blue magic ni nzuri zaidi naona inajaza
sana nywele, inalainisha, na kuzifanya zikae wiki nzima zikishine, coz mimi
huwa nikipaka jumapili sipaki tena hadi jumapil ingine na nywele huendelea
kulegea na kubaki katika mvuto wake
HIVYO NDIO VITU
NINAVYOTUMIA KICHWANI KWANGU
ADDITION
1. Usisubiri
harusi au sikukuu ndio uende salon, jitahidi kila wiki, au kama utashindwa basi
atleast mara mbili au tatu kwa mwezi
2. Kata
ncha za nywele zako kidogo kila baada ya miezi miwili unapotoka kuretouch
3. Usisuke
nywele siku chache baada ya kuretouch, utazikata, acha ziotee kwanza ndio
usuke,
4. Usifumue
nywele kama unagombana, fumua taratiibu, kama umesikuka kimasai basi ikibidi
chambua nywele moja moja kwa kutumia sindano,
5. Usipende
sana kutumia loterbody au jerry, hii inakata sana nywele labda kuwe na sababu
maalum ya kufanya hivyo, lakini, mh! Sishauri sana
6. Kwa
wale wapenda rangirangi kama mimi, unapoweka breach, usifikishe kwenye ngozi,
(shina la nywele) breach inapakwa kwa juu tu!
7. Pia
wale wa kutong, ni nzuri sana kutong kwa kutumia rolas au mabomba ya mipapai au
mirija ya juice, lakini kutong kwa kutumia mashine, sio kuzuri sna sababu
mashine inaunguza nywele,
8. Usiwejiweke
dawa mwenyewe kama sio mtaalamu au usimpe mtu asielewa namna ya kuweka dawa ,
atafanya zikatike, that’s whay unashauriwa kwenda salon,
Kuna uwekaji wa
aina mbili,
a) Kwa
wenye nywele nyingi na kavu hadi juu, unaporetouch anza chini, then katika
kuchanganya apake hadi juu ili kulainisha zile za juu,
b) Kwa
wale wenye nywele chache, na laini, unaporetouch usifikishe dawa juu
utazimaliza, weka dawa chini tu! Kule kuliko otea, na kama ni chache halafu
kavu, basi rambisha kidogo kwa juu dakika kumi au 15 kabla ya kuosha,
c) Jitahidi
unaporetouch usiwe na Mba nyingi kichwani, maana zinasababisha kuungua sana na
kung’oka nywele kutokana na majeraha,
PAMOJA
NA VYOTE HIVYO, NYWELE ZINAHITAJI USAFI SANA, ILI ZIPATE NAFASI YA KUKUA
VIZURI, HATA KAMA UMESUKA UNAWEZA KWENDA SALON UKAOSHA NA KUKAUSHA, HIZO NYWELE
ULIZOSUKA
Nimefurahi sana kwa maelezo yako,unaweza niambia nywele ngumu zinahitaji steaming ya aina gani?
ReplyDeleteAhsante kwa ushauriwako sasa nimeelewa sana juu ya utunzaji wa nywele
ReplyDeleteJaman mm siweka dawa ila hapo kwenye blue magic ni fire natumia hay mafuta mm bas nywele zangu nikizifumua zimejaa na ni ndefu sio poa
ReplyDeleteConditioner unatumia ya Aina gani
ReplyDelete